SAM-NCSMS ni mfumo jumuishi unaounganisha Uongozi wa Shule, Walimu, Wazazi na Wanafunzi kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya kitaaluma, kifedha na kimaendeleo kati ya wazazi na shule.
Tuma Ombi la Usajili Soma Zaidi
SAM-NCSMS ni mfumo wa kisasa zaidi uliojikita katika ubunifu wa mifumo ya usimamizi wa elimu nchini Tanzania kwa kurahisisha na kuboresha utendaji kazi wa shule kitaaluma na kifedha.
Tukiwa na lengo la kurahisisha na kuleta ufanisi kwenye taasisi za elimu, tumeunda mfumo huu ili kutatua changamoto za ukusanyaji ada, uandaaji wa matokeo na urahisi wa upatikanaji wake kwa wakati, ufuatiliaji wa ufundishaji/ujifunzaji, mahudhurio ya kila siku, na mawasiliano ya moja kwa moja kati ya shule na wazazi.
Usalama wa Data
Msaada wa Kutechnical
Nursery hadi Advance
Dira: Kuwa jukwaa namba moja la kiteknolojia linaloendesha shule zote nchini Tanzania.
Makao Makuu: Dar es Salaam, Tanzania
Barua Pepe: support@sam-ncsms.com
Subdomain Format: shule.sam-ncsms.duckdns.org
Usimamizi wa shule kwa ujumla, mwenendo kamili wa vyanzo vyote vya mapato ya shule (Ada (Kwa shule binafsi), Michango ya shule na Mapato ya ndani ya Shule), ripoti za maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi na mwenendo wa ufundishaji wa Walimu, Usimamizi wa Mawasiliano ya watumiaji wa mfumo wa shule na wazazi.
Kusimamia matokeo ya shule, ratiba za ufundishaji, mwenendo wa ufundishaji, usimamizi wa mitihani, mahudhulio ya wanafunzi kwa ujumla na Kutoa taarifa/Matangazo ya kitaaluma kwa walimu na wazazi.
Usimamizi wa Ada kwa shule binafsi, michango ya shule, mapato ya ndani ya shule na matumizi ya shule pamoja na utoaji wa taarifa na matangazo yanayohusu fedha za shule.
Ufuatiliaji wa karibu wa maendeleo ya wanafunzi wake anaowafundisha, urahisi wa uingizaji wa alama na takwimu za ufaulu, ufuatiliaji wa mahudhulio darasani kwa walimu wa darasa, usahidizi wa upatikanaji wa nukuu za kufundishia kulingana na mtaala mpa wa elimu ya Tanzania na utoaji wa taarifa za kimaendeleo kwa wazazi.
Kupata matokeo ya masomo kwa wakati, ulipaji wa ada (kwa shule binafsi), michango ya shule, madeni ya shule, nukuu za kujisomea wanafunzi warudipo nyumbani, ripoti za maendeleo ya kitaaluma (mahudhulio na mitihani) kwa wakati na kupata matangazo yote ya kimaendeleo ya shule kutoka kwa uongozi wa shule, mtaaluma, mhasibu na walimu.
Mfumo umezingatia ulinzi na usalama wa hali ya juu ambapo kila shule inajitegemea kwa kila kitu kwwnye mfumo na watumiaji wa shule husika tu ndio wanauwezo wa kutumia Mfumo.
Lead Systems Architect
Msimamizi mkuu wa ujenzi wa mfumo, mikakati ya kibiashara, na mwelekeo wa jukwaa la SAM-NCSMS.
Software & Security Engineer
Mtaalamu wa usalama wa mfumo, muundaji wa database, na usimamizi wa subdomains.
Jaza fomu hii fupi, na timu yetu itawasiliana nawe mara moja kwa ajili ya kuiweka shule yako kwenye mfumo.